Mgombea ubunge wa jimbo la Lushoto kwa tiketi ya Chadema, mkoani Tanga, Mohamed Mtoi amefariki baada ya gari lake kupinduka wakati akitokea kwenye kampeni jana jioni.
Akithibitisha taarifa hizi, Katibu wa Chadema wilayani Lushoto, Abdalah “Dula” Dhahabu amesema ajali hiyo imetokea jana jioni wakati mgombea huyo akitokea Mlola alipokuwa anafanya kampeni kuwania kiti hicho.
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment