September 11, 2015

Magufuli Azuru Kaburi la Nyerere Butiama.......Akabidhiwa Kifimbo cha Nyerere


Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akizuru kaburi la Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo, wilayani Butiama, Mkoa wa Mara jana , aliposimama kwa muda akielekea kwenye mkutano wa kampeni wilayani humo jana. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya.

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli akiweka shada la la maua alipozuru kaburi la Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo wilayani Butiama, Mkoa wa Mara, aliposimama kwa muda akienda kufanya mkutano wa kampeni wilayani humo.
 Msanii Dokii na Mwakilishi wa watu wenye ulemavu Aman Mpanju wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi hilo
 Dk Magufuli akiwasha mishumaa alipozuru kaburi hilojana
 Dk Magufuli, Waziri Mkuu wa zamani, Joseph Warioba, wasanii na  viongozi wengine wakiwa na mashada ya maua wakijiandaa kuweka kweenye kaburi hilo
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi mjini Butiama jana
 Baadhi ya wananchi wakiwa wamejikinga na kwa kutumia bendera wakati wa mkutano huo
 Dk Magufuli akiwanadi wagombea ubunge; Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) wa Jimbo la Musoma Vijijini na Nimrod Mkono wa Jimbo la Butiama
 Wananchi wakishangilia baada ya kumuona Dk Magufuli alipokuwa akihutubia na kujinadi katika mkutano huo wa kampeni mjini Butiama
 Profesa Muhongo akikabidhiwa Ilani ya Uchaguzi na Dk Magufuli. Pia Mkono naye alikabidhiwa Ilani hiyo
 Mgombea urais wa Ta nzania kupitia CCM, John Magufuli akikwasalimia wananchi huku akiwa na kifimbo alichozawadiwa na Wazee wa Kimila wa Kabla la Wazanaki wakati wa mkutano wkampeni wilayani Butiama alioufanya baada ya kuzuru kabila la marehemu Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Nyerere Nyerere katika Kijiji cha Mwitongo
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli  akimuonesha  Waziri Mkuu wa zamani, Jaji mstaafu Joseph Warioba kifimbo alichokabidhiwa zawadi na na Wazee wa Kimila wa Kabla la Wazanaki wakati wa mkutano wa kampeni wilayani Butiama alioufanya baada ya kuzuru kabila la marehemu Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Nyerere Nyerere katika Kijiji cha Mwitongo jana. Kulia ni Mjumbe wa  kamati ya kampeni za CC
 Dk Magufuli akiwasili kuanza kampeni katika mkoa wa Mara baada ya kumaliza katika Mkowa wa Tanga
 Dk Magufuli akimsalimia mtu mwenye ulemavualipowasili
 Dk Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, ShyRose Bhanji wakati wa mapokezi
 Chifu wa Wazanaki, Japhet Wanzagi akisalimiana na Dk Magufuli. Kulia ni Makongoro Nyerere
Dk Magufuli akikabidhiwa zawadi ya Kifimbo cha Mwalimu Nyerere wakati wa mkutano huo wa kampeni wilayani Butiama.
Mpekuzi blog

No comments:

Post a Comment