September 17, 2015

HAYA MAFURIKO YA MAGUFULI MKOANI KIGOMA APOKELEWA KAMA MFALME, MBUNGE WA KIGOMA MJINI KUPITIA CCM AKATALIWA MBELE YAKE...SHUHUDIAAA TU

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo. PICHA NA MICHUZI JR-KIGOMA.


Dkt Mafuli amewaabia wananchi wa Kigoma kwenye mkutano wa kampeni leo jioni kwenye uwanja wa kawawa kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema,amesema kuwa Serikali yake haitakuwa ya kunyanyasa mama ntile na kudaiwa kodi za hovyo hovyo,amesema kuwa ataimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali yake, lakini pia atawabana wafayabiashara wakubwa ambapo baadhi yao hawalipi kodi


Magufuli amewataka Wananchi kumuamini kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.


Maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.




Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo.


Aidha hadi tarehe 16 September 2015, Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, alikuwa amekwishafanya kampeni katika mikoa 12 na Majimbo 94. Amekwishafanya mikutano mikubwa ya hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari, jumla ya kilomita 13,720. Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na asilimia zaidi ya 30 ya wapiga kura.


Wananchi na Mabango yao

No comments:

Post a Comment