September 30, 2015

Dk. Cheni Afunguka Kumuoa Lulu!

Tangu wakati ule msanii maarufu wa filamu, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ aamue kupambana kumsaidia Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwenye kesi ya mauaji iliyokuwa inamkabali, yaliibuka madai kuwa wawili hao ni wapenzi lakini leo limeibuka la ndoa, Ijumaa lina kila kitu.

Madai ya uhusiano wa Lulu na Dk. Cheni yamekuwa yakienea chinichini kiasi cha kuwafanya baadhi ya watu kuamini kuwa, huenda lisemwalo lipo na kama halipo laja.


Lakini Cheni ana mke

Hata hivyo, madai hayo yanakuja ikiwa inafahamika kabisa kuwa, Dk. Cheni ana mkewe aitwaye Sabrina Zahrain ambaye wanaonekana kupenda licha ya kwamba imani yake haimzuii kuona mke wa pili.

Madai ya ndoa

Wakati tetesi za mastaa hao kuwa wapenzi zikizidi kushika kasi, hivi karibuni mtu wa karibu wa ‘wauza sura’ hao alilipenyezea gazeti hili umbeya kuwa, eti uhusiano wao umeshamiri na wana mpango wa kuona.

Chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake kilinyetisha kuwa, hata mashabiki wa wasanii hao wakisikia kuwa siku f’lani ndoa inafungwa wasishangae kwani ni jambo ambalo Cheni ameona siyo baya kwake.

“Ukaribu wa Lulu ni zaidi ya nyie mnavyojua, Cheni anaingia pale kwa Lulu masaa 24 na ninachojua Dk. Cheni anataka kumuoa Lulu mke wa pili, sasa kama mnataka kujua undani wa hili fuatilieni,” kilidai chanzo hicho.

Dk. Cheni atafutwa

Kufuatia madai hayo Ijumaa lilifanya jitihada za kuongea na Dk. Cheni ambapo alipopatikana alifunguka kama ifuatavyo:

“Hivi jamani mimi nikimuoa Lulu kuna shida gani? Yeye si mwanamke na mimi ni mwanaume, sasa tatizo liko wapi, hebu acha mambo yako bwana.

“Halafu ujue mimi ni Muislam naruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja. Hilo la kwenda nyumbani kwake ni kwamba pale naingia masaa 24, kwani nani wa kunizuia?”

Lulu anasemaje?

Ijumaa baada ya kuongea na Dk. Cheni lilimtafuta pia Lulu kupitia simu yake lakini hakupokea kila alipopigiwa na hata alipotumiwa sms hakujibu. Paparazi wetu pia akafika nyumbani kwake maeno ya Mbezi jijini Dar lakini akaambiwa na mfanyakazi wake wa ndani kuwa ameenda kwenye mishemishe zake.

Chanzo: GPL

No comments:

Post a Comment