September 6, 2015

CHEKI HAPA ALICHOANDIKA MH MAGUFULI MTANDAONI..DK CHACHE BAADA YA KUHITIMISHA KAMPENI NYANDA ZA JUU KUSINI



Tafsiri ya mabadiliko imeanza kupotoshwa, Lazma watanzania kwa pamoja tufahamu tunachokihitaji halafu tukitafute kwa nguvu tukipate. Wachina kwa sasa si taifa tena la Kubeza Duniani hawa walihitaji mabadiliko ya kweli wakayatafuta. Viongozi wao walitafsiri vizuri dhana hii ya mabadiliko na wakaamua kuyaleta kwa kutumia chama kile kile CPC.

Mabadiliko ya kweli yanaanzia kwenye fikra za anayetaka kuyaleta. Lazma wanchi wote tuwe na fikra chanya katika kuliendeleza taifa letu. Twende pamoja katika kuliendeleza taifa letu. Tunapaswa kushukuru waliotutangulia wamelifanyia mengi taifa hili.

Ni uongo wa mchana mtu kusema kwa miaka 50 hakuna kilichofanyika. Nina dhamira ya kulitoa taifa hili hapa lilipo na kupiga hatua nyingine kimaendeleo.

WATANZANIA NA WAPENDA MABADILIKO YA KWELI TUNAENDA KUSHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA MWAKA HUU. NIAMINI

**Mtu wa kazi na Vijana wa kazi**

No comments:

Post a Comment