September 14, 2015

BAUNSA WA MZEE YUSUF ALIVYOPIGWA RISASI

Mayasa Mariwata na Gabriel Ng’osha
HATARI! Jamaa maarufu kwa jina la Hassan Baunsa ambaye ni baunsa wa mwanamuziki wa Taarab Bongo, Mzee Yusuf ‘Mfalme’, amenusurika baada ya kupigwa risasi na shabiki aliyefahamika kwa jina mmoja la Kev, Ijumaa Wikienda lina mkanda kamili.
 Hassan Baunsa akiwa hospitali.
Tukio hilo la kutisha lilijiri juzikati kwenye Ukumbi wa Hugos uliopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro katika onesho maalum lililoandaliwa na kundi zima la Jahazi Modern Taarab chini ya Mzee Yusuf ndipo Kev alipojitokeza na kutaka kuingia ukumbini bila kulipia kiingilio kilichopangwa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, Hassan Baunsa alikuwa kwenye harakati za kumdhibiti jamaa huyo ambapo walikwaruzana kisha Kev akaondoka.Walisema kwamba, baadaye jamaa huyo alirejea kisha akalipa kiingilio na kuzama ndani.
Ilisemekana kwamba, wakati anataka kutoka ukumbini humo usiku mnene, Kev alirushiana maneno na Hassan Baunsa ambapo jamaa huyo alianza kwa kumpiga baunsa huyo ngumi shingoni kisha akatoa bastola na kumpiga risasi ya mkono wa kushoto.
Kutokana na ishu hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Mzee Yusuf ambaye muda mwingi simu yake haikuwa hewani ila meneja wake, Hans Kiumbe alisimulia tukio hilo kuwa liliwaacha midomo wazi kwa kuwa ni tukio la kustaajabisha mno.
Alisema baada ya msala huo kutokea huku Hassan Baunsa akitokwa damu, walilazimika kumuwahisha Hospitali ya KCMC kwa matibabu huku taratibu za kisheria zikichukua mkondo wake.“Hassan ni baunsa wetu ambaye kila shoo ya Mzee lazima awepo, tukio lile lilitusikitisha sana maana yule kijana ni mtemi huko Moshi kwa madai kuwa yeye ni mtoto wa dada wa mfanyabishara mkubwa hapa Bongo.
“Baunsa wetu alipomkataza kuingia kwa kumtaka alipe kwanza ndipo akachukia na kumpiga kibao, jambo ambalo Hassan hakukubaliana nalo.“Baadaye aliamua kulipa lakini alipokuwa anatoka ndipo akampiga Hassan ngumi kisha akatoa bastola na kumfyatulia risasi mkononi.
“Tulipotoa taarifa polisi walimkamata na kumtia ndani akisubiri sheria ichukue mkondo wake,” alisema meneja huyo.
Kwa sasa Hassan Baunsa anaendelea vizuri baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini. 

No comments:

Post a Comment