September 10, 2015

AJALI MBAYA..!! BASI LA PEACE MAKER LAGONGA NA KUUWA DEREVA BODABODA HUKO MJINI KAHAMA


Mwendesha pikipiki aliyefahamika kwa jina la Davidi Amoni umri (27) mkazi wa nyasubi wilayani kahama mkoani Shinyanga amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu baada ya kugongwa na Basi la kampuni ya Piece Maker.

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia kahamafm kuwa ajali hiyo imetokeaa leo saa 12 ya asubuhi katika eneo la faraja kata ya kahama mjini, ambapo dereva huyo wakati anajaribu kuingia katika barabara kuu ghafla aligongwa na basi hilo. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, basi hilo la Abiria aina ya scania lenye namba za usajili T 167 ARV, lilikuwa likiendeshwa na Bahati masanja (47) mkazi wa mwanza.

Akizungumza na kahamafm kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya halimashauri ya mji wa kahama Dk.George Masasi amesema marehemu huyo alipoteza maisha muda mfupi baada kufikishwa hospitalini wakati akipatiwa matibabu na madaktari.

Dk.Masasi amebaisha kuwa marehemu huyo amepoteza maisha baada ya kupata majera kichwani na mguu wa kulia kuvunjika hivyo kupelekea kuvuja damu nyingi ambayo zimesababisha kifo chake. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyan Justus Kamugisha amethibitisha kutoka kwa tukio hilo na kudai kuwa chanzo chake ni mwendo kasi wa madereva wote wawili, na kwamba dereva wa basi hilo amekimbia na wanaendelea kumtafuta.

No comments:

Post a Comment