Mbunge Mteule Millie Odhiambo akihutubia wanahabari awali. Picha/PHOEBE OKALL
MBUNGE wa Mbita Millie Odhiambo Mabona amemtaka mwanaume anayedai kuwa na picha zake akiwa uchi wa mnyama, kuthubutu kuzichapisha.
Katika makabiliano kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, mbunge huyo alisema hajali kuitwa kahaba. Mnamo Jumanne, Bi Millie alisema hajali jinsi watu wanavyofikiria kuhusu tabia zake.
“Nilijitosa katika siasa nikijua nitashambuliwa kuhusu masuala ya maadili, ngono na mengineyo,” alisema Bi Millie kwenye ujumbe wake.
Alimwambia mwanaume huyo, aliyetajwa tu kama Elisha, kuchapisha picha zozote alizonazo. Kulingana na Millie, mwanaume huyo alikuwa akitaka pesa kutoka kwake ili asizichapishe picha hizo anazodai zinamwonyesha akiwa tuputupu. Mbunge huyo alisema huo ni uzushi mtupu wala hapakuwapo picha zozote kama hizo.
“Nina kitu cha kuaibisha mikononi mwangu na kinaelekea kwa vyombo vya habari; kinaweza kukuchafulia jina kabisa na hata kuharibu taaluma yako ya siasa,” ulisoma ujumbe wa Bw Elijah, kwa mujibu wa ujumbe wa mbunge huyo wa Mbita.
Bw Elisha aliendelea, “Pamoja na picha kadhaa za uchi kutoka kwa jamaa ambaye huwezi kutarajia. Nitumie anwani yako ya barua pepe nikutumie ujionee. Ni dharura.”
Hata hivyo, Bi Millie hakuonekana kutishika. “Chapisha chochote hicho na 'haribu taaluma yangu’. Wewe wala yeyote hamwezi kuniteka na vitisho,” alimjibu Bw Elisha. Bi Millie, ambaye alikuwa amerejea juzi tu kutoka ziara ya wiki moja nchini Israel ya Kamati ya Kilimo ya Bunge, alisema hakuzaliwa mbunge na hatatishiwa na nia yoyote ya Bw Elisha, ikiwemo kuchapishwa kwa picha hizo za uchi.
“Watu wanatoa wapi wazo kwamba nitakufa nisipokuwa mbunge?” aliuliza kwenye ujumbe wake na kuongeza kuwa wanawake wa Kiluo hawana muda wa kupoteza kwa vitisho vya kipuuzi kama hivyo.
Kujua kazi
Mbunge huyo wa Mbita, ambaye alitumia maneno ya kubuni Nyaluo Oksechi – kumaanisha Waluo hawaombi mtu- alisema ana kazi yake ya uwakili ambayo alisema 'najua kuifanya vyema sana’.
Aliwaambia wakosoaji wake ambao hudai amepoteza umaarufu wake wa kisiasa – wakitumia neno 'Irumo’ kwa Kiluo – kwamba shutuma zao hazina msingi wowote.
“Ninamuogopa Mungu pekee. Sikupi pesa zozote. Chapisha chochote hicho kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari,” alimuambia mwanaume huyo kwenye Facebook.
Walipofanikiwa kuzungumza kwa simu, Bi Millie alisema mwanaume huyo, ambaye anazungumza kwa lugha za Kiingereza na Kiluo, alimwambia nia yake ni kumlinda.
“Iwapo ni yeye aliye na hicho kinachofaa kuniharibu, kwa nini nimpe pesa zozote?” aliuliza.
Ujumbe huo ulivutia mamia ya maoni huku viongozi kadhaa waliojumuika hapo wakimtia nguvu. Mbunge wa Rangwe George Oner alisema: Kila mtu huja hapa (duniani) uchi.” Mbunge wa Ndhiwa Agostino Neto alisema: “…dadangu, naweza kutoa maoni? Hebu mweleze tulikuwa majirani, sisi ni watu watajika Homa Bay ambao hatutishiwi na lolote.”
No comments:
Post a Comment