Staa mrembo wa Bongo Movies, Lungi Maulanga hivi karibuni ametoa ushuhuda wake kwamba alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kujisaidia kitandani mpaka alipofika kidato cha pili lakini alipona katika mazingira ya kushangaza.
“Nikiri tu kwamba nilikuwa kikojozi mpaka nafikia form two, nilikuwa naona aibu sana lakini aliyenisaida ni bibi mmoja ambaye aliniponya katika mazingira ya kushangaza.
“Baada ya kumwambia tatizo langu, aliniambia nipande kwenye mti wa muembe nikiwa na nguo zangu, nikiwa juu akaniambia nikojoe kisha nishuke.
“Niliposhuka, akaniambia nibadili nguo na kusema tatizo langu limeisha, sikuamini lakini ukweli ni kwamba kuanzia siku hiyo sikujisaidia tena kitandani.” Lungi aliliambia gazeti la Ijumaa
No comments:
Post a Comment