Show ya mwisho kufanya na marehemu sharo ilikuwa mwembe yanga show ya DTV nakumbuka ilikuwa inaitwa "NI WAKATI WAKO" baada ya hapo kesho asubuhi tukaenda tanga kushuti movie yetu hii (Safara Hasara) ambayo 20/04/2015 ndio inatoka tukamaliza kushuti salama salimini tukarudi DAR usiku napigiwa simu na marehemu sajuki anataka niende kwenye show yake iringa CHANGIA SAJUKI tarehe 25/11/2012 akabaki kwa sababu alikuwa katoka magomeni kaamia sinza ana siku mbili bado mgeni sinza basi mimi nikafanya show ya marehemu sajuki vizuri tu.
Tarehe 26 wasanii tunarudi kutokea iringa kuja dar kwenye msiba wa marehemu JOHN MAGANGA pia nae alikuwa msanii mwenzetu, nafika ubungo simu yangu inaita naangalia sharo nikapokea akiniuliza vipi bado mpo mbali nikamjibu nipo Ubungo akaniambia hata mimi pia nipo Ubungo naelekea Tanga kumuona mama jibu langu nikamuambia wewe si tumetoka tanga hata wiki bado na hivyo si unajua kwamba tunamsiba wa msanii mwenzetu jibu lake akaniambia kuna jambo muhimu hata na wewe mwenyewe shuka uje twende wote muhimu muhimu plz!.
Wakati mimi naangaaika kutafuta wapi gari yake ipo kwa muda nikawa sioni lakini yeye ananiona kumbe mwenzangu kaacha OPA kumbe kachukua gari nyingne ya Mudy Suma taa zinaruhusu sharo anatupita kwa ukatuni wake Sharo tunapishana sauti ya mwisho kwa kumuona macho kwa macho aliniambia say ooh! mamaaa......nafika msibani kwa John Maganga tumbo likanza kuniuma nikapitiliza home moja kwa moja.
Punde sms inaingia kutoka kwa sharo broo sipo poa nahisi kama nimerogwa hivi hayo yalikuwa maneno yake mwisho kupitia sms kuanzia tumbo likaanza kuchanganya kuuma mpaka saa mbili na dakika zake napigiwa simu ya msiba wa Sharo.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi ameen na kuanzia hapo ndio nikajua kwa nini Sharo alikuwa ananilazimisha tuwe na Stanbakora katika kazi zetu ilikuwa sio rahisi kiivyo mimi kumuelewa ingawaje kumbe mwenzangu alikuwa anamanisha....Show ya kufanya na marehemu ya sharo ilikuwa MWEMBE YANGA na show ya kwanza kufanya na Stanbakora ilikuwa MWEMBE YANGA ilikuwa ya E.fm
By Kitale

No comments:
Post a Comment