March 4, 2015

Wema Sepetu aamua 'kuolewa'. Aenda kumtambulisha mume nyumbani kwao.


Kwa mujibu wa tovuti ya Mange, inasemekana mwanadada Wema Sepetu ameamua kufanya kweli na kwenda kumtambulisha mume wako mtarajiwa nyumbani kwako Singida tayari kwa mipango ya ndoa.
Kupitia picha iliyowekwa kwenye tovuti hiyo, inayomuonesha mwanadada Wema akiwa na pete ya ndoa kidoleni anayodaiwa kuvalishwa na mchumba wake huyo ambaye wapasha habari wa hapa mjini wanadai ni yule tajiri wa Uganda - Ivan aliyekuwa mume wa mwanadada Zari ambaye kwa sasa ni mpenzi wa ex wa zamani wa Wema – Diamond Platnumz.
Wacha BongoMovie iendelee, Sisi yetu macho na masikio. Tunaisubiri ndoa hii kwa nguvu zote.
Unahisi Diamond na Zari watahudhuria kwenye harusi hii? Tupe maoni yako....

No comments:

Post a Comment