March 2, 2015

WAJUE TENA MASTAA WATANO WANAOTOKA FAMILIA ZA KISHUA HAPA TANZANIA



Hakuna mtu asiyejua maana ya watoto wa kishua basi kama yupo basi maana halisi ya neno hili ni wale watoto waliozaliwa kwenye familia zinazojiweza au unaweza kuita familia Bora. Mara nyingi wasanii wengi huwa wanatokea maisha duni na kupigana na maisha hadi kufikia walipo sasa. Kipindi Diamond akiacha shule kwa kukosa pesa ya kumsomesha nana elimu yake kuishia A’level , Hawa wengine walikua wapo shule wakisoma na kuishi vizuri. Vibe Tanzania inawaorodhesha baadhi ya watoto wakishua ambao kwasasa ni celebrities…


Vanessa MdeeVanessa Hau Mdee au unaweza kumuita Vee au Vee Money alizaliwa mjini Arusha mwaka 1988. Vanessa mdee alikuzwa na baba yake Sammy Mdee (kwasasa ni marehemu )ambaye alikua ni mtu mzito kwenye nchi hii na mama yake sophia. Akiwa na umri mdogo Vanessa aliweza kusafiri nchi mbalimbali duniani. Vanessa Mdee alikulia miji ya New York , Paris , Nairobi na Arusha.



NisherNisher ni mtoto wa Mtumishi wa Mungu Mh Nabii GeorDavie anayeongoza huduma ya Ngurumo ya Upako yenye makao yake jijini Arusha. Nisher amekulia katika maisha mazuri na hadi ni wakishua bado. Baba yake aliweza kumsaidia Nisher kufungua studio yenye thamani kama ya milioni 15 ili mtoto wake aendeleze kipaji alichonacho.

Jokate MwengeloHuyu unaweza kumuita mtoto wa Oysterbay kwani ndio alipokulia huku baba yake akifanya kazi serikalini. Kumbuka Jokate alizaliwa washington DC nchini Marekani ambapo wazazi wake walikua wakifanya kazi huko. Alipomaliza high school katika shule ya Loyola ndipo alipogombania Miss Tanzania mwaka 2006 na kushika nafasi ya 2.


LucciJina lake halisi anaitwa Luciano Tsere au unaweza kumuita Lucci ambaye ni producer maarufu nchini. lucci amezaliwa tarehe 30 September mwaka 1985 Lusaka Zambia, akiwa ni mzaliwa wa nne, wa mwisho kuzaliwa na akiwa mtoto wa kiume pekee kwenye familia yao. Lucci naye kama jokate amekulia Obey kwenye familia bora ambapo kwasasa mzee wake ni balozi wa Tanzania.


Wema SepetuWema Sepetu ni msichana anayetoka kwenye Familia ya kibalozi akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa Balozi Isaack Sepetu Ibrahimu (marehemu).Wema sepetu alizaliwa mnamo mwaka 1988 katika hospitali ya ST. Andrew’s jijini Dar es Salaam na ni mtoto wa mwisho kuzaliwa huku akisoma elimu yake ya primary na sekondari katika shule ya ACADEMIC INTERNATIONAL iliyopo jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Nchini Malaysia kusomea mambo ya biashara za kimataifa katka chuo cha Limkokwing University.

Wema mmeshaiona sana picha zake ndio maana hapa sijaiweka...

No comments:

Post a Comment