March 18, 2015

TAARIFA KAMILI KUHUSU KIFO CHA MDOGO WAKE JOSSE CHAMELEON WA UGANDA HII HAPAA ..R.IP AK47


AK47 kushoto akiwa na Jose Chameleone
Emmanuel Mayanja alimaarufu kama "AK47",mdogo wa mwanamuziki Jose Chameleone alikutwa ameanguka chooni na baada ya marafiki kugundua hilo ndipo walipomchukua na kukimbiza Hospital lakini bahati mbaya alifariki dunia njiani wakati akipelekwa Hospital ya Nsambya na walipofika hospital ndipo ikathibitika kuwa mwanamuziki huyo amefariki dunia.


Choo kinachodaiwa kuwa alianguka AK47 
Msanii Jose Chameleone wa Uganda akilia baada ya kumpoteza mdogo wake AK47.
AK47 ni baba wa watoto wawili ambao ni mapacha lakini pia ni mdogo kabisa wa msanii Jose Chameleone,Weasel na Pallaso.
 Jose Chameleone Amepost ujumbe Instagram
BongoSwaggz inatoa pole kwa Familia Ya Marehemu na wote walioguswa na msiba huu.

No comments:

Post a Comment