Staa wa Bongo Fleva na Bongo Movie,Shilole amedaiwa kutaka kumpiga tena mpenzi wake ambaye pia ni msanii Nuh Mziwanda kwa chupa hivi karibuni wakiwa kwenye sherehe ya kuzaliwa meneja wa msanii Kajala,aitwaye Lamata iliyofanyika pande za Samaki Samaki,Posta,jijini Dar.
Katika tukio hilo habari zinasema kuwa Shilole alikuwa amelewa sana na kwamba walikuwa wamekaa sehemu tofauti na Nuh Mziwanda,ghafla sehemu aliyokuwa amekaa Nuh na wasanii wengine ilirushwa chupa ambayo ilikuwa ikimlenga msanii huyo bahati nzuri aliikwepa ikampiga jamaa mmoja lakini haikumjeruhi.
Baada ya tukio hilo ilibidi baadhi ya wasanii wamuijie juu Shilole na kumuuliza kwanini alitaka kumpasua Nuh kwa chupa,Shilole alianzisha ugomvi na kuzua tafrani kwenye sherehe hiyo baadaye aliamua kukaa pembeni peke yake na kuanza kulia.
‘’Yaani unaambiwa kama ile chupa ingempata Nuh sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine alikuwa anamjeruhi vibaya sana kiukweli alileta fujo sana kwenye ile sherehe,"alisema mmoja ya watu walikuwa kwenye sherehe hiyo.
Baada ya hapo msanii Quick Racka alimfuata Shilole na kumwambia kuwa kumbe akilia anakuwa mbaya ndipo aliamka na kumrushia chupa ambayo kwa bahati nzuri Quick Racka naye aliikwepa ikapasuka chini.
Hata hivyo Soudy Brown kupitia Uheard alipompigia simu Shilole kumsomea mashtaka hayo alimwambia asimsumbue kwani kwa muda huo alikuwa amelala.
Shilole amekuwa akimpiga na kumdhalilisha mpenzi wake Nuh Mziwanda kwa kumpiga hadharani mara kwa mara ambapo miezi ya hivi karibuni alimpiga vibao kwenye tamasha moja lililofanyika pande za viwanja vya Leaders na baadaye kumuomba msamaha mpenzi wake kupitia vyombo vya habari na kuahidi kutompiga tena.
No comments:
Post a Comment