March 2, 2015

MREMBO BONGO MOVIES ATAMANI KUPATA MTOTO, AKOSA MWANAUME WA KUMPA.


Staa wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan amesema kuwa anatamani kupata mtoto wa pili kwa sababu mtoto wake wa kwanza amefikisha miaka 10, tatizo hana wa kuzaa naye.

Akipiga stori na Mwandishi Tiko alisema yeye ni ‘mgonjwa’ wa watoto wachanga na anahisi sasa ni muda muafaka ila tatizo mwanaume aliyenaye hana mpango wa kupata mtoto.

“Yaani acha tu, mpenzi niliyenaye naona kama hajajiandaa maana hata nikiongelea ishu ya kubeba mimba, naona ananipotezea lakini kiukweli nahitaji mtoto wa pili,” alisema Tiko.

Haya Wadau wa Zali la Mentali Mpo ?

No comments:

Post a Comment