March 4, 2015

MKE AMTANDIKA MUMEWE MAKOFI HADHARANI KISA HATOI ELA YA KUMTUNZA MTOTO..


waandishi wetu/mchanganyiko11
UPEPO umegeuka! Imani ya kwamba wanaume ndiyo wamekuwa wakiwapa kipondo wake zao imegeuka, safari hii mwanamke aliyejulikana kwa jina la Naomi Peter akimpa kipondo ‘hevi’ mumewe John Shila mchana kweupe!
Naomi Peter akitoa kipondo kwa mumewe.
Wawili hao wakazi wa Misheni, jijini Mwanza waliibua timbwili la aina yake ambalo liliwavuta watu wengi chanzo kikiwa ni mwanaume huyo kumkataa mtoto aliyezaa na mwanamke huyo.
Akizungumza na waandishi wetu, mmoja wa mashuhuda alisema wawili hao walioana na kuishi kama mke na mume na baadaye kupata mtoto mmoja wa kike, baada ya  miaka miwili ulitokea ugomvi na kusababisha mwanamke kuondoka na ndipo John alipotumia mwanya huo kuoa mwanamke mwingine.
Majirani wakiamulizia.
“Siku ya tukio, Naomi alimpeleka mtoto wake nyumbani kwa mzazi mwenzake kutokana na kutopewa hela ya matumizi, wakati huo Shila alikuwa na mwanamke wake mpya ndani, baada ya mabishano ya muda ndipo Naomi akaanza kumshughulikia Shila kwa kumtandika mangumi.
“Jamaa alikuwa hapeleki matumizi kwa mzazi mwenzie, mbaya zaidi alikataa na kudai mtoto si wake ndipo timbwili lilipoanzia,’’ kilisema chanzo hicho.
...Atimaye kipondo kikiendelea.
Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, wakati ugomvi huo ukiendelea mwanamke wa John wa sasa alikuwa kimya ndani na kushuhudia mpenzi wake akipokea kichapo kisha kumkabidhi mwanaye amlee na yeye akaondoka zake.
Hadi shuhuda wa habari hizi anaondoka eneo la tukio, muafaka juu ya kilichofikiwa ulikuwa bado haujapatikana.

No comments:

Post a Comment