March 14, 2015

HARUSI YAVUNJIKA BAADA YA BWANA HARUSI KUCHEMKA HESABU NDOGO TU ALIYOULIZWA NA BIBI HARUSI! ..ANGALIA USHANGAE

Kuna taarifa ambayo imepewa headlines, hii inahusu harusi moja kushindwa kufanyika India kisa ni kitendo cha bwana harusi kufeli swali la hesabu ya kawaida kabisa aliloulizwa na bibi harusi.

Walioshuhudia harusi hiyo wamesema bwana harusi aliulizwa swali hili;  kuwa ”15+6=?
Sherehe ya harusi hiyo iliharibika baada ya bi harusi kuanza kuongea kwa hasira baada ya kukasirishwa na kitendo cha mumewe huyo mtarajiwa kutoa jibu la hesabu hiyo kwamba ni 17.
india2
Bibi harusi aliondoka jukwaani akiwa amekasirika na kusema hawezi kuolewa na mtu ambaye hakwenda shule.
Ndugu wa bwana na bibi harusi walikubaliana kurudishiana zawadi zote walizotoa kwa ajili ya sherehe ya wapendwa hao.
Asilimia kubwa ya ndoa za India hupangwa na wazazi na mara nyingi maharusi hukutana kwa mara ya kwanza siku ya sherehe ya harusi yao.
Baba yake na bibi harusi, Mohar Singh aliyekuwa amepanga harusi hiyo katika kijiji cha Rasulabad alisema kuwa mwanawe alishangaa kuwa mumewe mtarajiwa Ram Baranhakuwa na elimu.

....CRDT MASAMA BLOG

No comments:

Post a Comment