February 26, 2015

MWALIMU AISHI NA KINYESI MIAKA MIWILI NDANI YA CHUMBA CHAKE CHA KULALA

Ama kweli dunia ina mambo, na ukistaajabu ya Mussa kweli utayaona ya Firauni kwa mwalimu huyu wa Sekondari ya Kibasila Jijini Dar Es salaam. Kwani katika hali isiyokuwa ya kawaida mwalimu Gaudensia Missanga mkazi wa Kisiwani kata ya Sandali wilayani Temeke anadaiwa kuishi katika chumba ambacho amehifadhi kinyesi hali ambayo inatishia usalama wa afya yake.

Hebu jenga picha, mwalimu wa shule ya Sekondari halafu anaishi ndani na kinyesi! Hivi hii imekaaje?
CLOUDS TV imeeona aah aah isiishie tu kusikia juu ya tukio hilo, imefika hadi kwenye nyumba anayoishi mwalimu huyo anayefundisha masomo ya sayansi na kuzungumza na mwenye nyumba REUBEN SHAYO ambaye ameeleza kilicho sababisha kubaini uchafu huo.
‘’Tuliona funza wakitoka chini ya mlango wake na harufu mbaya ikitoka na mwenzetu hatujawahi kumuona akioga wala akiingia chooni ndiyo tukabaini hali hii,’’alisema Shayo.
Kwa upande wake mwalimu GAUDENSIA anayetuhumiwa kuishi na kinyesi kinachodhaniwa kuwa ni cha binadamu hakuweza kupatikana kujibu tuhuma hizo na alipopigiwa simu yake ya mkononi ilikuwa inaita bila majibu.
Hadi CLOUDS TV inaondoka nyumbani kwa mwalimu huyo chumba chake kilikuwa kimefungwa huku taratibu zingine zikiwa zinaendelea.

No comments:

Post a Comment