January 20, 2015

Supu yasababisha Jamaa Kumuua Kaka Yake...........kisa kizima hiki hapa



Hii inatoka Nigeria, Sunday Osemwekhe alifikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji na amekubali kwamba alifanya kosa hilo, lakini chanzo cha ugomvi wao ilikuwa shutuma alizompa kaka yake kwamba alimuibia supu.

Ugomvi ukaenda mbali zaidi, Osemwekhe aliamua kuchukua panga na kumjeruhi kaka yake huyo semehu mbalimbali za mwili, ambapo baada ya kufikishwa Hospitali alifariki kutokana na majeraha makubwa.

Uchunguzi wa Polisi Nigeria umeonyesha kuwa mtuhumiwa alishikwa na hasira baada ya kuangalia supu yake aliyoiacha kwenye sufuria ya supu na kugundua haikuwa kama alivyoiacha, mzozo ukaanza kati yake na kaka yake, hasira zilipozidi Osemwekhe alichukua panga na kumpiga kaka yake na kumsababishia majeraha makubwa.

No comments:

Post a Comment