MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Rwanda Nzovwe jijini Mbeya , Elika Mkubwa (8), amefariki dunia baada ya kubakwa na watu wasiojulukana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alisema baada ya watu hao kufanya unyama huo, waliuweka mwili wa mtoto huyo katika sinki la kuogea kwenye nyumba moja ambayo haijakamilika ujenzi wake. Pamoja na hayo, alisema upelelezi bado unaendelea ili kuwabaini waliohusika na tukio hilo.
Akizungumza eneo la tukio, kiongozi wa Mtaa wa Ilomba, Ezekiel Mwakalandwa, alisema taarifa za mauaji hayo alizipata jana asubuhi kupitia kwa majirani zake.
Akizungumza eneo la tukio na paparazi huru, kiongozi wa Mtaa wa Ilomba, Ezekiel Mwakalandwa, alisema taarifa za mauaji hayo alizipata jana asubuhi kupitia kwa majirani zake.
"Nilipota taarifa hiyo, niliongozana na majirani tukiwa na ndugu wa marehemu na kushuhudia mwili wa mtoto huyo ukiwa umelazwa kwenye sinki la kuogea huku sehemu zake za siri zikiwa zimeharibiwa vibaya"
Mama mlezi wa mtoto huyo, Sala Mwandobo, alisema mtoto huyo alitoweka nyumbani kwake January 7 mwaka huu baada ya kuaga anakwenda kufua nguo za shule eneo la chemchem ya maji lililopo mbali kidogo na nyumbani kwake.
January 12, 2015
Home
/
MAAJABU
/
UDAKU
/
Mwanafunzi wa Darasa la Tatu Abakwa Mpaka Kufariki na Kutupwa Kwenye Sinki la Kuogea
Mwanafunzi wa Darasa la Tatu Abakwa Mpaka Kufariki na Kutupwa Kwenye Sinki la Kuogea
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment