January 30, 2015

"KUNA TATIZO GANI LIPUMBA KUPIGWA?.....NAWAPONGEZA SANA POLISI KWA KUMPIGA"---HII NI KAULI YA LUSINDE BUNGENI


Kulikuwa  na  mvutano  mkali  sana  bungeni  wakati  wabunge  wakijadili  hoja  ya  Lipumba  kupigwa. Hapo  chini  nimekuwekea  michango  ya  Lusinde  na  Sadifa  waliyoitoa  Bungeni:
  
Lusinde: Kwani kupigwa Lipumba ndiyo tatizo, wamepigwa viongozi wangapi hapa, Lipumba siyo wa kwanza kupigwa

Lusinde: Nawapongeza Polisi safari hii kapigwa muhusika mwenyewe, ndiyo nzuri hiyo, siyo wapigwe wengine, kupigwa kazini ndiyo sawa

Lusinde: Bunge linapokwenda mwishoni wabunge wenye hali mbaya majimboni wanakuwa na hamsha hamsha ili wafikiriwe

Lusinde: Nawashauri wapiga debe mkiona watu wanaandamana magari hayatembei hampati pesa na nyinyi andamaneni.
  
Sadifa: Mnasema Lipumba kapigwa, hajapigwa hapo, kaguswa tu, huwezi kumlinganisha Lipumba na Kikwete.
VIDEOM INAYOONYESHA LIPUMBA AKIPIGWA HII HAPA ICHEKI

No comments:

Post a Comment