January 20, 2015

ISIS WADAI FIDIA YA DOLA MILIONI 200 KUWAACHIA MATEKA WA JAPAN...

Video ikiwaonyesha mateka wa Kijapan, Kenji Goto Jogo na Haruma Yukawa, walio katika nguo za rangi ya chungwa, wakiwa na Jihadi John anayedai fidia ya Dola milioni 200 ili kuwaachia mateka hao.
Waziri Mkuu wa Japana, Shinzo Abe, ambaye anategemewa kuokoa maisha ya mateka wa Kijapan.
Kenji Goto Jogo (kushoto) mwandishi wa habari wa Japan na Haruna Yukawa mwanajeshi kutoka kampuni binafsi, wote walikamatwa nchini Syria mwaka jana.
 WAPIGANAJI wa Taifa la Kiislam (ISIS) wametoa picha za video ambapo linatishia kuwaua mateka wawili wa Kijapan kama hawatalipwa Dola milioni 200 (Sh. Bilioni 358) katika muda wa saa 72 zijazo. 

Mateka hao ni Kenji Goto Jogo mwandisi wa habari aliyekuwa anaandika kuhusu vita vya ndani vya Syria mwaka jana, na  Haruma Yukawa mwanajeshi kutoka kampuni binafsi aliyekamatwa nchini Syria mwezi Agosti mwaka jana. 

Tishio  hilo limekuja baada ya Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, kuahidi kutoa kiasi hichohicho cha fedha  kama msaada usiokuwa wa kijeshi kwa nchi zinazopigana dhidi ya ISIS. 

Video hiyo iliyosambazwa katika tovuti zinazohusiana na wapiganaji hao, ziliomwonyesha mpiganaji mwenye lafudhi ya Kiingereza ambaye anajulikana kama ‘Jihadi John’ aliyeonekana katika video za mauaji ya kuwakata vichwa mateka David Haines, Alan Henning (Waingereza), na  James Foley na Steven Sotloff (Wamarekani) hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment