January 19, 2015

Hii ndio zawadi ambayo Ray C amemwandalia Jakaya Kikwete



Rais Jakaya Kikwete ana mchango mkubwa kwenye maisha ya Rehela Chalamila aka Ray C. Kwa kutambua hilo, Ray C anatarajia kumpa zawadi maalum kwa moyo wake aliouonesha kuokoa maisha ya muimbaji huyo aliyewahi kuwa mtumiaji wa dawa za kulevya.

Ray C amekiambia kipindi cha The Mboni Show cha TBC1 kuwa hana zawadi kubwa zaidi ya kumpatia JK zaidi ya kuandaa show kubwa na kumkaribisha kuwa mgeni rasmi.

“Kwa ukweli sina uwezo wa ukweli wa kumpa chochote kile,” alisema Ray C. “Lakini nachojua kitu alichoniambia ni kwamba ‘nitafurahi sana ukirudi kwenye muziki na utaendelea na shughuli yako’ nikamwambia ‘baba nitafanya hivyo,” aliongeza.

“Kwahiyo nimeweza kurekodi album nzima na ninategemea nifanye show kubwa sana ambayo nitamwita yeye awe mgeni rasmi na nina uhakika siku atakayoniona kwenye stage atajua kweli nimerudi, kweli aliokoa kipaji. Maana yake ameokoa kipaji, watanzania walishanizoeana na nadhani ningeondoka kwa style ile nadhani ningewaumiza sana mashabiki wangu. Nashukuru nimerudi ni ni mzima wa afya.”

No comments:

Post a Comment