Wiki hii nataka kuzungumzia tabia f’lani ambayo imejengeka kwa baadhi ya wanaume ambayo kimsingi ni mbaya na haileti picha nzuri lakini naamini kwa kuandika kupitia safu hii, itasaidia kuwafanya wahusika wabadilike.
Natambua umuhimu wa watu kukutana sehemu mbalimbali na kubadilishana mawazo, haijalishi ni eneo gani ambalo litatumika. Wapo ambao stori zao huzipigia baa na wengine maskani tu. Huko ndiko tunakojadili mambo kadha wa kadha yanayogusa maisha yetu ya kila siku. Mimi nadhani ni jambo la msingi sana kwani naamini watu zaidi ya mmoja wanapokutana na yanayozungumzwa yakawa ni yenye maana, ni lazima yatakuwepo mabadiliko chanya kwa wahusika.
Lakini pamoja na yote hayo, nimegundua kuna baadhi ya wanaume wanapokuwa kwenye mazungumzo kama hayo huingia pia katika kuzungumzia maisha yao ya kimapenzi na baya zaidi ni kwamba, badala ya kuzungumzia mambo mazuri huingia kwenye kuzianika kasoro walizonazo wapenzi wao. Jamani huu si ulimbukeni uliopitiliza?
Yaani wanafanya hivyo wakiwa na imani kwamba eti kwa kuzieleza kasoro hizo, wenzao watawasaidia katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao. Unaweza kumsikia jamaa akisema mbele za watu;
“Unajua kuna kitu kinaniumiza kichwa sana washikaji, mpenzi wangu hayajui kabisa mapenzi, yaani nikiwa naye faraha naona kama niko na gogo vile!” Labda nikuulize wewe msomaji, kwa mtu mwenye busara anaweza kweli kuanika kasoro hiyo kwa wenzake?
January 3, 2015
CHUMBANI ZAIDI: SIRI ZA MPENZI WAKO FARAGHA ZINAWAHUSU NINI RAFIKIZO?!
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment