January 31, 2015

AUNT EZEKIEL IYOBO HAWEZI NIPA MIMBA MIMI....NIKIJIFUNGUA NITAMTAJA BABA WATOTO




KAMA kawaida wadau wa safu bora kabisa ya Sindano Tano, kutokana na maombi yenu leo tumemleta yule mwanadada kipenzi cha wengi Aunt Ezekiel amefungukia maswali matano.

Mwanadada kipenzi cha wengi Aunt Ezekiel.

Paparazi: Mambo vipi? Kwema lakini Aunt? Ehne leta maneno, mna mipango gani na baba mtoto mtarajiwa, Iyobo?
Aunt: Hahaha mimi mzima! Kuhusu Iyobo, mh! Kanipa mimba! Si kweli, nitakapojifungua nitamtaja baba wa mtoto wangu.

Paparazi: Mbona Iyobo amekuwa akijinadi kwenye vyombo vya habari kuwa mzigo ulionao ni wake?
Aunt: Mh! Jibu langu ni hilo nililokupa.

Paparazi: Msanii gani wa kike ambaye unamkubali sana Bongo.
Aunt: Kwa kweli namkubali sana Wema Sepetu.

 
Aunt Ezekiel akiwa na Mose Iyobo.


Paparazi: Hivi kabla ya kuingia kwenye ‘u-miss’ ulikuwa unafanya shughuli gani?
Aunt: Nilikuwa nishaanza uigizaji ndipo waandaaji wa mashindano ya u-miss waliponiona na kuniambia nafaa na baada ya hapo nikashiriki kule Ilemela, Mwanza.

Paparazi: Ukiambiwa utoe ushauri juu ya penzi la shemeji yako wa zamani Diamond kwa mpenzi wake wa sasa Zari, utawaambiaje?
Aunt: Hahaha! Jamani hapo kwa kweli ‘no comment’.

No comments:

Post a Comment