WAANDISHI wa habari wa mjini Dodoma, wamenusurika kushambuliwa kwa kipigo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kongogo, Daud Husein baada ya waandishi hao kubaini maonevu na ubabe anaowatendea wananchi.
Mwenyekiti huyo, aliwashabulia waandishi kwa matusi na maneno makali huku akiwabeza kuwa ni makanjanja kwa madai kuwa wasingeandika kero za wananchi bali matendo yake.
Alisema kuwa waandishi hao walitakiwa kuwapuuza walalamikaji kwa madai kuwa aliwakarimu waandishi, hivyo hawakuwa na sababu ya kuandika uozo wake. Hali hiyo ilijitokeza kabla kuanza kwa mkutano wa kijiji cha Kongogo na vijiji vya jirani ambao lenga lake lilikuwa ni kupinga mradi wa ujenzi wa lambo la kunyweshea mifugo ambalo wananchi wanalipinga wakidai hawajashirikishwa.
Kwa pamoja wananchi wa vijiji vya Tinahi, Asanje, Babayu na Kongogo walisema mtendaji wa kijiji cha Kongogo amekuwa akiwaburuza na kujiamria mambo yake.
No comments:
Post a Comment