October 1, 2014

MPYA!! HAWA NDIO NYOKA 10 AMBAO NI HATARI SANA DUNIANI USIACHE KUWAJUA HAPA


Ijapokuwa jamii yote ya viumbe hawa huchukuliwa kama ni hatari kwa binadamu, ukweli  ni kwamba hawana madhara makubwa kiasi hicho tena kuna baadhi ya binadamu wanawatumia kama mifugo ya ndani.


Hata hivyo kuna baadhi ya nyoka ambao wapo katika kundi maalum kutokana na ukali wa sumu zao, kama sumu zao zikiingia ndani ya mwili wa binadamu ni kitendo cha sekunde kadhaa maisha yanakatishwa.

Ifuatayo ni orodha ya nyoka kumi ambao wana sumu kali zaidi duniani-:
NAMBA 1 Anaitwa  Rattlesnake

Mkia wake unamfanya awe wa pekee zaidi, rattlesnake  yupo katika familia ya pit viper. Baadhi ya nyoka wa jamii hii wana sumu aina ya hemotoxic ambayo kama ikiwekwa kwa mhanga wa nyoka huyu itasababisha kudhoofu kwa viungo, kuharibika kwa tishu za mwili na kuharibika kwa damu (kuganda kwa damu).

Rattlesnake wana uwezo wa kugonga umbali mrefu wa zaidi hata ya mara mbili ya mwili wake, kwahiyo kuwa makini kama ukikutana na mmoja hakikisha haupiti karibu yake. Na kama ikitokea kwa bahati mbaya ukagongwa na nyoka wa jamii hii mwenye sumu kali zaidi kama vile “eastern diamondback”  tegemea kushindwa kupumua vizuri, kupooza, kuvuja damu kwa ndani. Utahitaji prompt antivenin ili kuweza kuongeza asilimia zako za kuishi 

NAMBA 2 Anaitwa Black Mamba


Black mamba wanapatikana kwa wingi katika maeneo mbalimbali ya bara la afrika. Inasemekana nyoka huyu ndio nyoka mwenye kasi zaidi kati ya nyoka wa nchi kavu akiwa anafika 12m/hr (mita kumi na mbili kwa lisaa). Pia anajulikana kwa kushambulia kwa usahihi na nguvu kubwa, na kwa kuongezea ana uwezo wa kugonga mara kumi na mbili kwa mpigo mmoja kana kwamba hivyo vyote havitishii sumu ya black mamba ina kitu kinaitwa post-synaptic neurotoxin na ana uwezo wa kuidunga kwa ujazo wa 1/250 oz, kiasi hicho kinatosha kusababisha kifo kwa asilimia 50%, Ikiwa itatokea umegongwa na nyoka huyu basi utapata homa, kutokwa na udenda kupitiliza, lakini pia misuli ya mhanga wa nyoka huyu itakuwa inafanya kazi kinyume na utaratibu, mfumo wa upumuaji pia utafeli kufanya kazi hivyo basi kupelekea kifo ndani ya dakika 15 hadi saa 1 tangu kuingia kwa sumu ya black mamba mwilini.

NAMBA 3 Anaitwa Anaconda


Jamii ya nyoka huyu ni star wa kwenye filamu nyingi za kutisha, kiasi kwamba kuna filamu ambayo imepewa jina lake na kama umewahi kushuhudia filamu hiyo basi jua kuwa ni kweli na ni mkubwa kiasi hicho na ndio ana uwezo wa kummeza binadamu kama alivyo. Ijapokuwa hana sumu kabisa (joka la kibisa) anaconda bado ni nyoka hatari kutokana na ukubwa wake, anaconda mkubwa zaidi kuwahi kuonekana alikua na urefu wa wa futi 28 (yaani Hasheem Thabeet kama wanne hivi waunganishwe) na unene wa inchi 44. Uzito uliokadiriwa ni kilo 226.79 sawa na uzito wa binadamu wanne wa kawaida. Staili ya anaconda ya kuua ni kwa kujivingirisha kwenye mwili wa mhanga wake kisha kumminya hadi kumvunjavunja na kumtoa pumzi yote. Lakini anaconda wana tambaa taratibu mno hivyo una nafasi ya kumuona akiwa mbali na kukimbia lakini fanya hivyo kabla hajafanya shambulizi la kukushtukiza

NAMBA 4 Anaitwa Viper

Viper aina hatari ya nyoka hawa wanaishi katikati na kusini mashariki mwa bara la asia na mashariki ya kati. Wana sumu ambayo kama ikiingia mwilini mwa binadamu itasababisha maumivu makali, uvimbe, na kubadilika kwa rangi ya mwili. Dalili za kawaida zinazo ambatana na madhara ya sumu hii ni kutokwa na damu kwenye fizi, kupungua kwa mapigo ya moyo, na shinikizo la damu la kushuka. Maumivu yanaweza kusalia kwa kipindi cha wiki 2 hadi 4, na kama usipotibiwa utaishia kupata mshtuko wa moyo au kifo kutokana na damu kuwa na sumu (septicemia death)

NAMBA 5 Anaitwa Death Adders



Wanapatikana Australia na New Guinea, nyoka huyu ana sumu kali mno na ni miongoni mwa nyoka wenye shabaha kali zaidi. Ana uwezo wa kukudunga ujazo wa gramu 180 kwa pigo moja. Sumu hiyo ina uwezo wa kusababisha kudhoofu kwa mwili haraka haraka lakini pia na kufanya mfumo wa upumuaji usiendelee kufanya kazi. Ijapokuwa kuna tiba ya sumu ya nyoka huyu ambayo imesababisha kushuka kwa asilimia ya vifo vinavyosababishwa na nyoka huyu.
Maumbile yao huwa ni wafupi, vichwa vya pembe tatu na meno ya chini na pia ni nyoka warefu zaidi nchini Australia

NAMBA 6 Anaitwa Philippine Cobra



Wanapatikana kaskazini mwa nchi ya philipino, kobra huyu ndie mwenye sumu kali zaidi ya kobra wengine. Matokeo ya sumu ya nyoka hawa ni kupooza kwa mfumo wa neva za mwili na upumuaji ambayo inafanya kupumua kuwe kwa shida. Lakini madhara mengine ni pamoja na maumivu ya kichwa, kutapika, kuharisha, kichefuchefu na maumivu ya tumbo pia yatajitokeza. Kifo kinaweza kukuta ndani ya dakika 30 tokea kung’atwa na nyoka huyu, kuwahi kufa huku ndio kunasababisha nyoka huyu awe na hatari kubwa.

NAMBA 7 Anaitwa Tiger Snake



Nyoka huyu ni miongoni mwa reptilia wakali zaidi ambao wanapatikana kule Australia. Inasemekana kwamba ndio nyoka wenye sumu ambayo ni hatari zaidi. Sumu yake ina presynaptic neurotoxins na procoagulants, ambayo kama ikiwekwa kwenye mwili wa binadamu inasababisha kupooza na kuishiwa nguvu kwa misuli ya binadamu na pia huingiliana na vitamin K ambayo inahusika na kugandisha damu na kupelekea kutokwa na damu bila kuganda.

NAMBA 8 Anaitwa Eastern Brown Snake



Nyoka huyu anapatikana kwenye nchi za Austrlia, Indonesia na Papua New Guinea. Usidanganywe na jina lake ambalo linaonekana la kawaida mno, kwasababu sumu ya nyoka huyu inasababisha madhara makubwa baadae. Sumu ya nyoka huyu inasababisha kupooza, renal kushindwa kufanya kazi, na mshtuko wa moyo. Kiasi kidogo tu cha 1/14,000 ounce moja kinatosha kuchukua maisha ya mtu mzima mmoja, kama utakutana nae basi hakikisha hupepesi hata ukope kwasababu nyoka huyu anafanya shambulia kutokana na mitikisiko ya kiumbe ambacho kipo karibu yake.

NAMBA 9 Anaitwa  Inland Taipan
 



Australia ni nyumbani kwa nyoka wenye sumu kali zaidi nyumbani na nyoka huyu ni miongoni mwa wale wengi ambao wamo nchini humo. Anachukuliwa kama nyoka hatari zaidi duniani kwasababu pigo moja tu la sumu ya nyoka huyu anae sisimua hadi uti wa mgongo lina uwezo wa kuua hadi binadamu 100. Sumu yake ambayo ina mchanganyiko mzito wa neurotoxic ina uwezo wa kushambulia mfumo wa neva kwa haraka na kuuharibu kabisa, amejipatia umaarufu wa kuwa nyoka wa ardhini mwenye sumu kali zaidi, dalili za kung’atwa na nyoka ni pamoja na kutapika na kupooza. Bahati nzuri ni kwamba ni nadra mno kukutana na nyoka huyu kwasababu huwa na aibu kubwa mno na mara nyingi hujificha kwenye nyufa za majabali na kwenye misitu. 

NAMBA 10 Anaitwa  Belcher’s Sea Snake
 


Nyoka huyu ana rangi ya manjano, mwili mwembamba na urefu wa kawaida juu kidogo ya futi 3. Nyoka huyu wa baharini anaweza kuonekana ni mwenye tabia nzuri na mara nyingi huwa hatoi sumu pale anapong’ata, lakini utashangazwa na jinsi gani sumu yake ilivyo na uwezo wa kuua, milligram chache tu zinatosha kuua watu 1000 (elfu moja), hii ina mfanya nyoka huyu awe hatari zaidi ya nyoka mwenye sumu kali zaidi kwa nchi kavu Inland Taipan. 
CREDIT SHEDDYCLASSIC

No comments:

Post a Comment