MNENGUAJI wa bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’, Aisha Ramadhani Mbegu maarufu kama ‘Aisha Madinda’, hivi karibuni anadaiwa kufanyiwa kitu mbaya baada ya kupokonywa pasipoti na simu zake kisha kubadilishiwa kazi aliyokusudia kuifanya na kufanywa hausigeli.
Asha anayejulikana pia kama Iron Lady, aliendelea kuweka wazi kuwa baada ya Aisha kufanyiwa hivyo hakuwa tena na uwezo wa kuwasiliana na mtu yeyote zaidi ya waliomteka, ila yeye alipata habari hizo baada ya kuwauliza baadhi ya wasichana wanaofanya kazi huko waliomwambia kuwa tokea wawepo Dubai hawajawahi kumuona wala kusikia habari zake.
Aisha aliondoka nchini hivi karibuni kwenda huko kwa ahadi ya kwenda kunengua katika kumbi mbalimbali za starehe, lakini ndoto zake zikayeyuka.

No comments:
Post a Comment