October 31, 2014

MLEGEZO WAMPONZA CHID BENZ MAHAKAMANI..DUH CHEKI POLISI WALICHOFANYA


Kuonesha wapo ‘serious’ na mavazi, polisi walimtaiti staa wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ na kumtaka akavae vizuri kisha arejee mahakamani. 
Tukio hilo lilitokea juzi, Jumanne katika Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, wakati staa huyo alipokuwa amefikishwa kusomewa mashtaka yake ya kukutwa na madawa ya kulevya.
Akiwa katika viunga hivyo vya mahakama, Chid Benz alionekana akiwa ametinga jinzi ambayo ililegezwa mkanda na alipoingia ndani ya chumba cha mahakama, mlegezo uliongezeka zaidi hadi kufikia chini ya makalio kitendo ambacho polisi walishindwa kukivumilia.

Kuonesha kwamba hawakufurahishwa na kitendo hicho, maafande waliokuwa wakimsindikiza Chid mahakamani hapo, walimtaiti kwa kumshika kiunoni na kumtoa nje kwenda kumpandisha suruali hiyo kisha kumrudisha akiwa amevaa vizuri.
Akiwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Waliarwande Lema na mwendesha mashtaka, PP Mwanaamina Komba, Chid alisomewa mashtaka matatu aliyokutwa nayo Oktoba 24, mwaka huu katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar. 
  
Mashtaka hayo ni; kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin gramu 0.25 yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi gramu 1.72 ambayo thamani yake ni Sh. 1,720 na vifaa vya kuvutia (kifuu cha nazi na kijiko).

Chid aliyakana mashtaka yote matatu hakimu akaahirisha kesi hiyo hadi Novemba 11, mwaka huu na kuweka dhamana wazi ya faini ya shilingi  milioni moja na wadhamini wawili lakini mshtakiwa hakukidhi masharti ya dhamana, akaomba kukamilisha masharti hayo kesho yake (Jumatano) hivyo akarudishwa mahabusu Segerea.

No comments:

Post a Comment