Baba wa binti mmoja amemkaripia binti yake wa miaka 10 kupitia mtandao wa kijamii Facebook kutokana na kitendo cha binti huyo kuongopea umri wake, kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na pia kuwa na akaunti za mitandao ya kijamii kitu ambacho hakiruhusiwi kwa mtoto wa umri kama wake.
Kali zaidi ni kuwa karipio hilo limeambatana na picha ambayo baba huyo amempiga picha binti yake akiwa amevalia tisheti yenye maelezo yanayoelezea umri wake pamoja na daraja la darasa analosoma.
Picha hii imeenea na kuchukua umaarufu sana mitandaoni siku ya leo.
No comments:
Post a Comment