Ndoa ya binti aliyetambulika kwa jina moja la Husna (16), imebuma baada ya bwanaharusi, Rahim (30), kuingia mitini muda mfupi kabla ndoa kufungwa.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, OFM walitinga kwenye sherehe hiyo na kuanza kuwahoji baadhi ya ndugu ambao walikiri kwamba kweli ile ilikuwa ni ndoa ya mtoto aliyeacha shule akiwa kidato cha pili.
Akizungumza na OFM, Husna alisema aliamua kuolewa kwa sababu aliacha shule kutokana na kukosa ada.
“Niliamua kuachana na shule maana nilikuwa sielewi chochote kwa sababu niliugua mapepo, nimeamua mwenyewe kuolewa jamani maana sina kazi ya kufanya,” alisema Husna.Baada ya baadhi ya watu kuwashtukia OFM, walimpa taarifa bwanaharusi kwa simu na hakuonekana na ndoa hiyo ikaishia hewani kwani jamaa huyo hakufika kwa kuhofia hilo.
Baada ya ndoa hiyo kubuma, mtoto Husna aliangua kilio huku akisema kwamba anampenda huyo mchumba’ke huku mama yake naye akiangua kilio akidai anaumia kwani hajui atakapozitoa hizo fedha za mahari shilingi laki nne kwani kipato chake ni kidogo.

No comments:
Post a Comment