October 22, 2014

Ali Kiba amewataja Wasanii waliomfurahisha kwenye stage ya Fiesta Leaders....


Ni week ambayo imefatana na weekend iliyoacha kumbukumbu nzuri kwa watu mbalimbali waliohudhuria tamasha la Fiesta ambalo mwaka huu limechukua headlines za rekodi kubwa ya mahudhurio karibu kila sehemu lilikopita ambapo Dar es salaam idadi inagonga kwenye elfu 50.

Ali Kiba alikua miongoni mwa wakali waliokubali mwaliko wa kutokea juu ya jukwaa hilo ambapo millardayo.com na AyoTV zilipata nafasi ya kuongea nae Exclusive aelezee ni Wasanii gani waliomvutia baada ya kuonyesha kazi zao on stage.
Ameanza kwa kusema >>> ‘Nilichelewa kufika sikuweza kuwaona kina Ommy Dimpoz, Vanessa na kina Young Killer lakini niliobahatika kuwaona wote wamefanya kazi nzuri, nilimkuta Waje na Panto walifanya vizuri japo ni nyimbo zao chache tunazijua’
Akiwataja wasanii wa Tanzania waliofanya vizuri Ali amesema >>> ‘Mr Blue amenifurahisha sana, WEUSI wamefanya kazi nzuri…. kina Diamond wamefanya kazi nzuri pamoja na Linah’

Credit:Millardayo.com

No comments:

Post a Comment