September 13, 2014

WASTARA STAREHE YANGU KUBWA SANA NI MAPENZI......HAPA KUNAFULL STORI.


Mwigizaji wa filamu Bongom, Wastara Juma akipozi.

NIWASHUKURU WOTE TULIOANZA NAO MAKALA HAYA AMBAYO MWIGIZAJI WASTARA JUMA AMEKUWA AKIFUNGUKA KUHUSIANA NA MAISHA YAKE, BILA SHAKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE TUTAKUWA TUMEJIFUNZA KITU KUPITIA MAISHA YAKE.


Leo tunamalizia sehemu ya mwisho ya makala haya, tutaona jinsi gani alikutana na aliyekuwa mumewe, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’. Twende pamoja:
Mwandishi: Ulikutana lini na Sajuki na wapi?
 Wastara: Nilikutana na Sajuki mwaka 2007 kwenye kazi ya filamu ambapo tulikuwa marafiki sana, mara nyingi tulikuwa tunakaa na kuzungumza stori za maisha huku kila mmoja akimweleza mambo aliyopitia katika mapenzi, ile filamu ilipoingia tu sokoni tukaanzisha uhusiano kwani kila mtu alikuwa na ‘stress’ za mapenzi na kila mmoja alikuwa ameshajua anachokipenda na anachokichukia mwenzake. 
Wastara: Kwa hiyo uhusiano tuliuanza rasmi mwaka 2008 ambapo tulikaa mpaka 2009 ndipo tukafunga ndoa, kabla ya ndoa wakati tukiwa tunaenda kulipia ukumbi mimi na Sajuki, tulipata ajali nikavunjia mguu. 
Wastara Juma akiwa na aliyekuwa mume wake marehemu, Sajuki JumaKilowoko.
 Mwandishi: Maisha ya ndoa kwa Sajuki yalikuwaje?
 Wastara: Ukweli yalikuwa mazuri kwani alikuwa ni mwanaume ambaye nilikuwa namhitaji kwani alikuwa na sifa zote, alikuwa ananipenda na ananijali kwa kila kitu lakini ndiyo hivyo Mungu amemchukua.

Mwandishi: Mpaka sasa kwenye kampuni yenu (WAJEY) mna filamu ngapi?
 Wastara: Tuna filamu 16 na za kushirikishwa ni 9 na nimeshirikishwa chache sababu mara nyingi Sajuki alikuwa anapenda tucheze za kwetu tu. 

Mwandishi: Ni kitu gani kizuri ambacho kiliwahi kukutokea na hutakisahau maishani? 
Wastara: Siwezi kusahau siku niliyopata Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike kutoka Global Publishers kupitia gazeti la Risasi kwani mpaka sasa hajawahi kutokea mwingine hivyo najiona niko bora mpaka leo.

Mwandishi: Katika maisha yako starehe yako kubwa ni nini?

No comments:

Post a Comment