Mtu mmoja ambaye ni dereva aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T. 495 ALM aina ya Nissan Pick Up amefariki dunia katika ajali mbaya huku mtoto wake akijeruhiwa vibaya maeneo ya Nane Nane hapa jijini Mbeya usiku wa kuamkia jana Septemba 01,2014 majira ya saa saba za usiku.
Dereva huyo aliyefariki dunia amefahamika kwa jina la Boniface Mwasoba alifariki dunia baada ya gari hilo kuacha njia na kupinduka katika maeneo hayo ya Nane Nane ajali iliyopelekea pia kujeruhiwa kwa mtoto wake anayefahamika kwa jina la Willy Boniface Mwasoba mwenye miaka 7 na mwanafunzi wa shule ya msingi Mkapa na amelazwa katika hospitali ya Rufaa jijini Mbeya.
Mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika japokuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi ili kubaini, lakini kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto kwa kuzingata sheria na alama za usalama wa barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
September 2, 2014
SHOCK AJALI MBAYA MBEYA MTOTO AJERUHIWA BABA APOTEZA MAISHA PALEPALE
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment