September 25, 2014

POMBE YAMAPANDISHA UENDAWAZIMU BINTI WA CHUO AFANYA MAAJABU NA WANASIKINDE NGOMA YA UKAE

BINTI mmoja wa chuo  aliyeonekana kuzidisha kiburudisho, mwishoni mwa wiki iliyopita alitibua onyesho na kugeuka kuwa burudani baada ya kupanda juu ya jukwaa la Mlimani Park ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’ na kuwakumbatia ovyo wanamuziki.
Binti akivamia jukwaa baada ya kupiga urabu wa kutosha.
Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita katika ukumbi wa Railway Club ambako paparazi wetu alimshuhudia binti huyo aliyefahamika kwa jina moja la Fatma, akianza kubadilika taratibu kadiri alivyokuwa akipata kiburudisho chake kilichokuwa katika vipakti vya plastiki.
Akizidi kusumbua jukwaa.
Licha ya kuwakumbatia, pia msichana huyo alivuruga shoo hiyo baada ya kukanyaga nyaya zinazounganisha vyombo vya muziki vya bendi hiyo na kusababisha umeme kuzimika jukwaani, hivyo kusababisha onyesho kusimama kabla ya mafundi mitambo kurekebisha hitilafu.

No comments:

Post a Comment