Bella na Banana wakikamua.
Matonya akitoa sapoti kwa vibao vyake kikiwemo cha 'Vailet'.
Ommy Dimpoz akikamua.
Mashabiki wakijimwaya.
Bella akikamua.
Papaa Thom Diamond, akimmwagia Ommy Dimpoz noti nyekundu.
Bella baada ya kuwaambia mashabiki anayempenda mama yake anyooshe mkono juu.
Mashabiki wakijifunika kava za viti baada ya mvua kuanza kutibua mambo.
Bella na Ommy Dimpoz wakiimba kibao cha ‘Nani Kama Mama’.STORI/PICHA NA: RICHARD BUKOS / GPL
MKALI wa muziki wa dansi hapa nchini, Christian Bella, Jumamosi usiku alizindua albam yake ya ‘Nani Kama Mama’ ambapo umati mkubwa wa mashabiki ulijitokeza kwenye onesho hilo lililofanyika Ukumbi wa Mzalendo Pub, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
Katika onesho hilo Bella alisindikizwa na Bendi yake ya Malaika Musica pamoja na wanamuziki wa kizazi kipya, Ommy Dimpoz, Banana Zorro na Matonya. Ingawa mvua ilitaka kuharibu mambo kwenye eneo hilo lililokuwa wazi, mashabiki waliofurika ukumbini hapo walikomaa mwanzo mpaka mwisho.
No comments:
Post a Comment