MKAZI wa Kijiji
cha Karundi, Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa, Moses Kang'ombe (17), amehukumiwa
adhabu ya kuchapwa viboko 20 baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji na
kusababisha mimba.
Hukumu hiyo imetolewa
juzi na Mahakama ya Wilaya hiyo baada ya kumtia hatiani
katika makosa mawili la ubakaji na kusababisha mbakwaji ambaye ni mwanafunzi wa
darasa la saba (jina tunalihifadhi), kupata mimba na kushindwa kufanya mtihani
wa kuhitimu mwaka huu.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ramadhani Rugemalila, alisema mshtakiwa alikiri kosa hivyo Mahakama ilimtia hatiani chini ya kifungu cha 130 (1) na (2)( e) na 131 (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.
Alisema katika kosa la kubaka, atachapwa viboko 12 na kosa la kumpa mimba mwanafunzi huyo, atachapwa viboko vinane.
Awali Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Hamimu Gwelo, aliiambia mahakama hiyo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo mwaka huu na baada ya mwanafunzi huyo kukutwa na mimba.
Aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa mshtakiwa iwe fundisho kwa wengine wenye tabia ya kuwabaka wanafunzi na kuwasababishia mimba.
Mahakama ilitoa adhabu hiyo kwa kuzingatia umri wa mshtakiwa mwenye miaka chini ya 18.

No comments:
Post a Comment