Kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza tuhuma za upendeleo katika utoaji nafasi za ajira 200 kwa watu walioomba nafasi hizo kupitia idara ya uhamiaji imebaini kuwa nafasi hizo zimetolewa kwa upendeleo bila ya kufuatwa taratibu, kanuni na sheria ya utoaji wa ajira hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi Mbarak Abdulwakil amesema kamati hiyo imeweza kubaini kuwa mambo mengi yalifanywa kiujuma jumla sana na hivyo kutoa mwanya wa watu kupindisha mambo.
Kamati hiyo iliundwa Agosti Mosi mwaka huu, chini ya watu watano ikiongozwa na yeye mwenyewe katibu mkuu wa wizara ya hiyo.
Pia katika mkutano huo jeshi la polisi kupitia mkurugenzi wa makosa ya jinai kamanda Isaya Mngulu amesema jeshi hilo litafanya operesheni ya kuhakikisha inawakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wakiwemo waganga wa kienyeji wanaojihusisha na vitendo vya kuwaua ama kuwajeruhi walemavu wa ngozi kwa imani zao za kishirikina.
August 22, 2014
SAKATA LA UHAMIAJI LACHUKUA SURA MPYA!!!!WAHAHA KUMTAFUTA MCHAWI NANI
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment