“Sina rafiki, yaani hivi unavyoniona mimi ndo hivi ninavyotoka hapa nyumbani, nyumbani shughuli zangu. Sipendi kuweka marafiki, marafiki sio watu wazuri kabisa. Yaani sipendi ndo Mungu alivyoniumba.” Amesema.
“Yaani zile tu labda kazini kuna msichana labda nafanya nae kazi ile ‘mambo poa basi’. Lakini ile ‘shoga sijui tutoke twende out..’ sitokagi kwenda club, sitokagi kunywa pombe. Sinywi, siwezi kuenjoy sehemu kama hizo kwa sababu sio mlevi. Raha ya mlevi uwe na mlevi mwenzako sasa mimi sio mlevi. Mara nyingi mimi napenda kukaa nyumbani kufanya mazoezi na dancers basi.” Ameeleza.
Meninah amesisitiza kuwa anachokieleza ni ukweli na kwamba kama kuna msichana ambaye ni rafiki yake basi ajitokeze.
Sikiliza mahojiano yote hapo kufahamu mambo mengi kuhusu muziki wake, uhusiano wa mapenzi na mengine mengi.

No comments:
Post a Comment