August 21, 2014

MAAJABU SASA..DEREVA BODABODA MBARONI KWA KUMNG’ATA MWENZAKE MDOMO NA KUONDOKA NAO.




DEREVA wa bodaboda, Adinan Adam, mkazi wa Kata ya Olorieni, mkoani Arusha ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumng’ata mdomo Shabani Temba na kuondoka nao.
Kijana Shabani Temba aliyepigwa na kung'twa na dereva wa bodaboda, Adinan Adam.
Akizungumza kwa uchungu wakati akitoa maelezo katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Olorieni, Shabani alisema ameshangazwa kujikuta anapigwa kisha kung’atwa mdomo na kutolewa nyama ya mdomo pasipokuwa na kosa lolote.
Temba alisema, Alhamisi iliyopita, majira ya saa 12 jioni alifika katika kijiwe cha vyuma chakavu katika kata ya Olorieni akiwa amechoka kutokana na mizunguko yake, ndipo alipoona akae juu ya bodaboda iliyokuwa imeegeshwa kijiweni hapo huku watu wengine wakiwa pembeni yake.
“Nilipokuta pikipiki (bodaboda) hiyo ikiwa imeegeshwa katika kijiwe hicho kutokana na hali yangu ya kuchoka, niliamua kuikalia ndipo ghafla mtuhumiwa alipotokea na kuanza kunishambulia kisha kuning’ata hadi kuondoa nyama yote ya mdomo wangu,” alisema mlalamikaji huyo.
Mtuhumuiwa ambaye ni dereva wa bodaboda, Adinan Adam(aliyesimama) akiwa Kituo Kidogo cha Polisi cha Olorieni, mkoani  Arusha

No comments:

Post a Comment