Ulichokuwa ukisubiri kwa muda mrefu huenda kikatokea hivi karibuni. Collabo ya Alikiba na Diamond Platnumz mabibi na mabwana inanukia.
Akizungumza na kipindi cha Jahazi cha Clouds FM leo (20/8), Alikiba amesema upo uwezekano wa kufanya kazi ya pamoja kama kukitokea mabadiliko.“Mawazo ya kolabo yapo, mawazo unapata mengi tu, hiyo nimeshaisikia vilevile, na wewe sio mtu wa kwanza kuniuliza hicho kitu kipo.
"Lakini muziki vile vile kama unavyoona kuna mavazi na style, vazi hili linatakiwa liende disko hili ni vazi la beach, vazi hili la ofisini, vazi hili la mpirani, hili la mchangani, hili la kwenye ukumbi unajua vitu kama hivyo!
"Kwahiyo Diamond akipata vazi lake ambalo linahusiana na vazi ambalo natakiwa nivae, hakuna tatizo tunafanya kazi kama kawaida, kwa sababu yeye anafanya kazi vizuri,” alisema AliKiba.
Alipoulizwa kama kuna uwezekano wa kufanya show kubwa na Diamond alijibu kwa kicheko: “Wewe hujui kama watu wanasubiria (show) au unajisahaulisha.”
August 22, 2014
Home
/
Unlabelled
/
KAMA WEWE NI SHABIKI WA ALIKIBA AU DIAMOND HII INAKUHUSU SANA! NI KUHUSU COLLABO LAO!!!!
KAMA WEWE NI SHABIKI WA ALIKIBA AU DIAMOND HII INAKUHUSU SANA! NI KUHUSU COLLABO LAO!!!!
Tags
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Related Posts:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment