| mtoto akiwa amehifadhiwa ktik mfuko wa rambo |
| hapa ndipo alipofichwa mtoto huyo |
| Hivi ndivyo mwanafunzi huyo alivyomhifadhi mtoto huyo |
| Mwenye chumba akiomba msamaha |
| Damu ya mtoto huyo aliyeuwawa |
| Polisi wakimhoji binti mwenye chumba |
| Hii ndio nyumba ambayo binti huyo alikuwa akiishi mwenye nyumba akiwa chini ya ulinzi akitolewa nje ni huyo mwenye sweta |
| Watuhumiwa wakitolewa katika chumba hicho |
| Polisi wakiweka ulinzi mkali |
| Mwanafunzi huyo akipanda katika gari la polisi |
| Mwanafunzi huyo akiwa na mwenyeji wake kushoto |
| Huyu ndie binti mwanafunzi aliyetuhumiwa kufanya mauwaji |
| Wananchi wakimtazama mwanafunzi huyo |
Tukio hilo la kinyama limetokea leo saa 12 jioni katika eneo la Kijiweni kata ya Mvinjeni Manispaa ya Iringa kutokana na baadhi ya majirani kufichua siri hiyo nzito ya kuwepo kwa jaribio za binti huyo kufanya mauwaji hayo.
Mmoja kati ya majirani aliueleza mtandao huu wa matukiodaima.co.tz kuwa binti huyo mwanafunzi akiwa na mimba ya miezi tisa alifika katika nyumba hiyo kwa rafiki yake ambae ni mfanyakazi wa bar mmoja eneo la vibanda vya CCM mjini Iringa aliyefahamika kwa jina la Joys siku kama tano kabla ya usiku wa jana kujifungua salama katika chumba hicho.
Shuhuda huyo alidai kuwa mapema asubuhi ya leo walisikia sauti ya mtoto mchanga akilia huku sauti ya radio ikipandishwa kupoteza sauti ya mtoto huyo ili wapangaji wengine wasijue suala hilo.
Hivyo kutokana na hali hiyo ndipo waliamua kufika ofisi za mtandao huu kufichua siri hiyo kwa maombi ya kutotajwa popote jina la shuhuda huyo.
" Mimi ni raia mwema na mwanamke mwenye uchungu nimekuja kwako huku nikijua hutatoa siri hii ...katika nyumba ambao naishi kuna mwanafunzi amejifungua mtoto jana usiku na kwa sasa amejifungia ndani na mwenye chumba anaitwa Joys anafanya kazi vibanda vya CCM sasa lengo la kujificha nafikiri ni kutaka kufanya jaribio la kuua mtoto huyo sasa naomba usaidie kuokoa maisha ya mtoto huyo unatusaidiaje na sisi kwenda polisi tunaogopa ushahidi"
Kutokana na maelezo hayo yasio na chembe ya uongo mtandao huu ulipiga simu kwa OCD Iringa Bw Pyuza na bila kuchelewa kikosi kazi akiwemo askari wa dawati la jinsia kilifika katika ofisi za mtandao huu wa matukiodaima na safari ya kufuatilia suala hilo ilipoanza kwa kumkamata mwenyeji wa mwanafunzi huyo ambae ni mmiliki wa chumba kisha kupokonywa simu yake ili asifanye mawasiliano nyumbani na baada ya hapo kwenda katika nyumba husika .
Hata hivyo ukweli wa jambo ulianza kujionyesha baada ya kufika katika chumba hicho na kukuta mlango umefungwa kwa ndani na baada ya mwenye chumba kugonga ndani mwanafunzi huyo aliigiza kuwa alikuwa akifanya usafi ila baada ya kuhojiwa na polisi alidai kuwa kwa sasa ana mtoto mmoja ambae yupo kijijini Magulilwa wilaya ya Iringa .
Uchunguzi wa kipolisi ulianza na kikosi hicho kwa maswali ya kiuchunguzi na ndipo alipokiri kuwa anamtoto mwingine ambae amejifungua usiku wa leo na amemhifadhi katika mfuko wa rambo ndani chini ya kitanda .
Alipotakiwa kumtoa alifanya hivyo na polisi na mmiliki wa mtandao huu kushindwa kujizuia kuangua kilio kutokana na kile walichokiona kutoamini .
Mtoto huyo alikutwa amekufa huku akiwa amefungwa na nguo nyingi pamoja na kumwagiwa vumbi ya mkaa na chumvi ili asitoe harufu na kufungwa vizuri katika mfuko wa rambo mweusi kisha kuwekwa katika mfuko mkubwa wa salfeti tayari kwa kuvuta subiri ya kwenda kumtupa mtoto huyo porini .
No comments:
Post a Comment