CHAMA cha ACT Wazalendo leo kimetoa ratiba yao kwa wanahabari kuhusu
kutangaza wagombea wake wa urais katika Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba
2015.
Ifuatayo ni taarifa yao kwa wanahabari:
Ndugu waandishi wa Habari
Karibuni kwa mara nyingine katika makao makuu ya Chama chetu.
ACT Wazalendo tunaendelea kuwashukuru kwa kuitikia wito wetu kila mara
tunapowaita kwa ajili ya kuchukua habari na kuzifikisha kwa umaa, hili
linatutia moyo na tunawashukuru sana
Ndugu Waandishi wa Habari
Tumewaiteni leo tukiwa na mambo Machache Muhimu kwa chama chetu na Taifa
kwa ujumla ambayo tungependa mtusaidie kufikisha kwa umma.
Julai mosi mwaka huu Chama Cha ACT-Wazalendo kilifungua rasmi pazia la
uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi mbali mbali za uongozi, kwa ajili
ya kuwawakilisha wananchi katika majukumu ya kiserikali.
Nafasi hizo ni kuanzia Udiwani Ubunge na Urais ambao kitaifa wawakilishi
hao watapatikana Oktoba 25 baada ya kupigiwa kura na wananchi.
Ndugu waandishi wa habari
Tangu kuanza kwa uchukuaji huo wa fomu kumekuwa na mwitikio mkubwa wa
wanachama wetu kuchukua fomu hizo. mapaka sasa kuna baadhi ya majimbo na
kata zina watia azma kuanzia wanne mpaka tisa hili ni jambo la faraja
kwetu.
Kati ya majimbo 265 yakiwamo majimbo mapya 26 yaliyoongezwa hivi
karibuni na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), ACT-Wazalendo tumeshakuwa na
waweka azma zaidi ya mmoja katika majimbo 226 kwa nchi nzima na
tunaamini mpaka kufikia mwisho wa uchukuaji fomu ndani ya Chama majimbo
yote 265 yatakuwa yanawatia azma mbali mbali wanaosubiri kupitishwa na
chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
Kichama mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu kwa nafasi ya udiwani ni
julai 24, kwa nafasi ya Ubunge mwisho julai 31 na nafasi ya Urais mwisho
wa kuchukua na kurudisha ni Agosti mosi.
Ndugu waandishi wa habari
Mwisho wa uchukuaji na urudishaji wa fomu hizo utafuatiwa na vikao mbali
mbali vya uteuzi kwa ngazi husika kabla ya kufika katika ngazi ya
Taifa.
Kwa ngazi ya Taifa Halmashauri kuu itakutana Agosti 13 kwa ajili ya
kuteua jina la mgombea Urais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
pamoja na kupendekeza majina ya wagombea Urais kwenye mkutano mkuu.
Agosti 13, Mkutano mkuu utamchagua mtu atakayepeperusha bendera ya Chama
cha ACT Wazalendo katika mbio za urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Tarehe hizo pia zianaweza kusogezwa mbele kwa sababu maalum na uamuzi
unaweza kufanywa Sekretariti ya Chama baada ya kukaimu baadhi ya
majukumu ya kamati kuu
Ndugu waandishi wa habari.
Pamoja na mafanikio yote tunayopata ACT-Wazalendo lakini pia kuna watu
bado wanatufanyia michezo michafu kwa kuwarubuni na kuwahadaa watu wetu
waliotia azma ya kugombea nafasi mbali mbali hususan maeneo ambayo
mawasiliano yana matatizo.
Hivi karibuni tumepokea taarifa kutoka katika miji ya Tarime na Rorya
Mkoani Mara kuwa kuna watu wanapita na kutangaza kuwa Chama chetu
kimezuiwa kushiriki Uchaguzi kwa muda wa miezi sita.
Tumebaini lengo la upotoshaji huu ni kuwakatisha watanzania tamaa juu ya
ukuaji wa Chama Cha ACT-Wazalendo pamoja na dhamira yake nzuri ya
kuirudisha nchi katika misingi iliyoachwa na hayati Mwalimu Julius
Nyerere.
Tunawataarifu wananchi kuwa Chama chetu kitashiriki uchaguzi mkuu wa
Oktoba 25 mwaka huu kwa kuweka wagombea wa nafasi zote na Chama
hakitakuwa tayari kuona sehemu yoyote ya nchi mgombea wa CCM anapita
bila kupingwa.
Ndugu waandishi wa habari.
Pia katika mkutano wetu wa leo tunapenda kuwatambulisha wanachama wetu wapya walio mbele yenu
Hawa ni Msanii maarufu wa filamu nchini Mohamed Mwikongi “Frank” na Mwingine ni Deo Meck
Deo Meck kabla ya kujiunga na ACT Wazalendo alikuwa mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi.
Kwa pamoja hawa wameungana nasi kwa ajili ya kuendeleza uzalendo kwa Taifa lao nasi tunawakaribisha.
Pia tendo hili la leo la kuwakaribisha vijana hawa ni mwanzo wa
kuwatambulisha wanachama mbali mbali wakiwemo wabunge na viongozi wa
vyama waliojiunga nasi baada ya kuvunjwa kwa Bunge.
Tayari tunao baadhi ya watu waliokuwa wabunge na wameshajiunga nasi na
mchakato wa kuwatambulisha unaendelea katika maeneo mbali mbali nchini.
Nawashukuru kwa kunisikiliza
Msafiri Mtemelwa
Naibu Katibu Mkuu,ACT Wazalendo
Julai 16/2015

No comments:
Post a Comment