May 15, 2015

"NILISHAWISHIWA SANA KUCHEZA FILAMU ZA UTUPU" -Mtoto Mzuri SABBY ANGEL wa Bongo Movies Afunguka!

Ni matumaini yangu mpenzi msomaji wa safu hii kwamba uko poa na unaendelea na majukumu yako vizuri. Leo tunamleta kwenu msanii wa filamu, Sabrina Omary ‘Sabby’ ambaye alibanwa kwa maswali 10 na Mwandishi Wetu IMELDA MTEMA, fuatilia… 

Ijumaa: Mara nyingi umekuwa siyo mtu wa kutulia nchini kwani muda mwingi unakuwa Nairobi, nini siri ya safari zako?
Sabby: Unajua robo tatu ya maisha yangu ni Nairobi kwani nimekulia huko na nimefanya vitu vingi nikiwa huko, ndiyo maana mara nyingi nakuwa huko. 

Ijumaa: Wewe ni msichana mrembo sana je, ni changamoto gani ulizokutana nazo ulipoingia katika tasnia ya filamu?
Sabby: Changamoto kubwa ni baadhi ya wanaume kutaka kunitumia kama Big G. 

Ijumaa: Vipi kuhusu uhusiano wenu wa kimapenzi na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Bob Junior uliishia wapi?
Sabby: Nafikiri kila mmoja hakuwa na malengo thabiti na mwenzake hivyo tuliamua kila mmoja achukue hamsini zake.

Ijumaa: Je, ni mwanaume gani sahihi unayemhitaji katika maisha yako?
 Sabby:  Mwenye kujali na kunithamini, kuhusu pesa ni kitu cha mwisho kabisa katika mapenzi.

Ijumaa: Siku hizi mastaa wengi hawajali kuolewa bali wanatafuta mtu na kuzaa naye, vipi kwa upande wako?
Sabby: Mimi nina mtoto tayari wa kiume, nampenda sana na kwa sasa ana umri wa miaka minne.


Ijumaa: Ukimpata mume wa maisha yako, unahisi ni kitu gani utakifanya?
 Sabby: Ukweli najivunia kwamba najua kupika kila aina ya chakula na ninaamini mwanaume yeyote anapenda kupikiwa vizuri, mimi uchawi wangu pamoja na mambo mengine utakuwa kwenye mapishi.

Ijumaa: Ulishawahi kuwa na uhusiano na staa yeyote wa kiume wa Bongo Movies?
Sabby: (Ndiyo), lakini sipendi kumtaja jina na tuliachana muda mrefu sana. 


Ijumaa: Unafikiri kama atajitokeza msanii kutoka Bongo Movies akataka kukuoa itakuaje?
Sabby: Sitaki kabisa maana siwezi tabia zao ni ngumu sana na hatuwezi kudumu kwa sababu kuna usemi usemao mafahari wawili hawaishi zizi moja. 

Ijumaa: Je, ulishawahi kushawishiwa kucheza filamu za utupu?
Sabby: Kuna jamaa mmoja alishanieleza jambo hilo nikiwa Marekani lakini nilimwambia mila na desturi zetu hazikubali vitu hivyo. 

Ijumaa: Mara nyingi mastaa wa Bongo Movies mnalalamikiwa kuiba waume za watu, unazungumziaje hilo?
Sabby: Ni kweli tabia hizo zipo na hiyo inatokana na mastaa wengi hatuolewi hivyo inawabidi wabanane hapohapo.

No comments:

Post a Comment