MAMA Fanueliii! Mwanamke Elgiva Winyaeli
Munisi ‘ Manka’ , mkazi wa Kijitonyama , Dar,
amejikuta katika wakati mgumu baada ya
mumewe , Alpha kudaiwa kuzinasa picha za
utupu akiwa na mchepuko uliofahamika kwa
jina la Crama Lucas ambaye ni msanii wa
Bongo Muvi , Ijumaa Wikienda lina filamu
kamili.
Elgiva Winyaeli Munisi ‘ Manka ’ na mchepuko
wake Crama Lucas ambaye ni msanii wa
Bongo Muvi , wakipozi kimahaba.
Chanzo makini kimeliambia gazeti hili
kwamba, awali , mwanaume huyo alizibamba
picha chafu za mwanaume peke yake zikiwa
kwenye laptop ya mkewe ambapo
alipomuuliza alijitetea si zake ni za rafiki yake
alimtumia yeye kupitia Mtandao wa WhatsApp .
MUME AJIONGEZA
Iliendelea kudaiwa kuwa , mume alimuuliza
rafiki aliyetajwa ambapo awali alikataa
kumtumia picha hizo Manka , lakini baadaye
alikiri jambo ambalo mume alijiongeza
akiamini lilipangwa .
MACHALE YAMCHEZA
Ilidaiwa kuwa , mume alimkalisha mkewe na
kumwambia alichofanya ni kosa kubwa katika
ndoa, mambo yakaisha.
Chanzo kilitiririka: “ Lakini mume akawa bado
machale kama yanamcheza kwani aliingiwa na
wasiwasi mkubwa kuamini kuwa , mkewe
anaweza kuhifadhi picha chafu za mwanaume
kwenye laptop.
“ Siku moja , mumewe alikwenda kwenye
stationery ( duka la vifaa vya kuandikia)
inayomilikiwa ya dada yake Manka (jina
tunalo) maeneo ya Sinza-Mori (Dar ).
“ Alipofika aliwauliza wafanyakazi kwamba
mkewe akienda pale hukaa kwenye kompyuta
gani ! Wakamwonesha , akakaa , akasachi jina la
mkewe likatokea folda lenye picha kibao za
mkewe huyo akiwa na Crama tena kwenye
mapozi ya kimahaba .
MUME APAGAWA
“ Palepale mume alipagawa, kidogo presha
imshike. Alimpigia simu mkewe akamuita aje
pale alipo lakini mke alisema ana kazi nyingi
nyumbani hawezi kutoka . Mume alitoka hadi
nyumbani kwake na kumuuliza mke wake
kuhusu picha hizo , mke akadai mwanaume
huyo ni mteja wake wa mashuka ! Mh !
“ Hasira zilimpanda mwanaume , mteja gani wa
mashuka hadi kupiga picha ? Alimpiga mkewe
hadi kumpasua sehemu ya paji la uso na
kumchomea nguo moto . Mke akakimbilia
Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘ Mabatini ’ , Dar
kushitaki lakini baadaye alifuta kesi. ”
MUME ASAKWA
Baada ya madai hayo , Ijumaa Wikienda
lilimsaka Alpha , alipopatikana alikiri kuwepo
kwa mgogoro kati yake na mkewe chanzo
kikiwa ni hizo picha chafu alizopiga mkewe na
zile alizopiga akiwa na mwanaume anayedaiwa
kuwa ndiye mchepuko wake .
“ Awali, nilizifuma picha za utupu za
mwanaume nikaamua kumpeleka mke wangu
kwao akapumzike lakini wazazi wake
walimuonya, akarudi tukawa tunaendelea na
maisha , sasa sijui amekumbwa na nini mpaka
leo hii akatoka nje ya ndoa wakati mimi nipo
na ukizingatia ni mtu ambaye nimetoka naye
mbali.
“ Mpaka nazikuta hizi picha sikuamini kabisa
kama mke wangu anaweza kunifanyia hivi .
Sijui walipigaje kwanza , lakini niliumia sana
nikaamua kumpiga mpaka akachananika usoni
na nilimchomea nguo zake zote kwa sababu
nilikuwa nina hasira . ”
MUME BADO
“ Tangu siku hiyo mke wangu aliondoka
nyumbani, mpaka sasa hivi anaishi kwa dada
yake lakini kila nikimuomba arudi nyumbani
anakataa na kudai kuwa anaogopa nitampiga ,
ila nilishaongea na yule mwanaume na
nikamtaka tuonane akaniambia hawezi
kuonana na mimi .
“ Pamoja na yote , bado ninampenda mke
wangu kwani sitarajii kufunga ndoa na
mwanamke mwingine , ” alisema Alpha.
Kuhusu uhai wa nyumba yao , Alpha alisema
alifunga ndoa na Manka mwaka 2009 katika
Kanisa la Anglikana Chimuli , Dodoma.
CRAMA ASAKWA
Kwa upande wake, Crama alipotafufwa kwa
simu na gazeti hili kuhusu madai hayo ,
alisema:
“ Mimi na Manka tunafahamiana kwa muda
mrefu tena ni rafiki yangu kwa sababu
tulifahamiana kupitia Mtandao wa Kijamii wa
Instagram na alikuwa akinikopesha mashuka .
“ Alikuwa anakuja sana nyumbani kwangu
kudai madeni yake lakini yeye mwenyewe
ndiyo alikuwa akinishinikiza tupige picha tena
kwa kutumia simu yake.
“ Sikujua kama ni mke wa mtu wala yeye
mwenyewe hakuwahi kuniambia kama
ameolewa na wala hakuwa na pete ya ndoa,
ila nilishawahi kumwambia kuwa picha
tunazopiga zisije zikazua balaa baadaye,
hakuonesha mshtuko.
“ Niliwahi kupigiwa simu na mume wake akidai
kuwa nilikuwa nikimuibia mke wake , kumbe si
kweli kwa sababu Manka mwenyewe
anamfahamu mchumba wangu . ”
HUYU HAPA MANKA
Manka alipotafutwa juzi kujibu tuhuma hizo
kupitia simu yake ya mkononi alidai kuwa
hawezi kuzungumzia suala hilo kwa muda huo
mpaka atakapojipanga:
“ Siwezi kuliongelea hilo sasa hivi mpaka pale
nitakapojipanga na kujua hizo picha zimefikaje
hapo ofisini kwenu. ”

No comments:
Post a Comment