December 6, 2014

ROSE NDAUKA AWAFUNGUKIA LIVE VIDUME VINAVYOMTAKA ..CHEKI HAPA


Mtoto mzuri Bongo Movies, Rose Ndauka.
MTOTO mzuri Bongo Movies, Rose Ndauka amewatega mashabiki wake kwa kutupia picha ya kidole chake chenye pete ya uchumba kwenye mtandao wa Instagram kuashiria kuwa amechumbiwa.
Mara baada ya paparazi wetu kuiona picha hiyo iliyozua mjadala mkubwa mtandaoni, alimtafuta Rose na kumtaka afunguke kama amechumbiwa upya baada ya kumwagana na aliyekuwa mchumba’ke, Malick Bandawe hivi karibuni. Msikie alivyojibu:
Kidole cha Rose Ndauka kikiwa na pete ya uchumba.
 “Kweli picha ni yangu, mimi ndiye nimeiweka, kuchumbiwa ni jambo la kheri lakini siwezi kusema kama tayari au bado, muda ukifika nitawaambia.”

No comments:

Post a Comment