Tumezoea kusikia watoto wakizaliwa na uzito wa kilo mbili na nusu hadi tano lakini hii inaweza kuwa sehemu ya maajabu kwani si rahisi mama kujifungua mtoto mmoja na si mapacha mwenye uzito mkubwa kama huyu aliyezaliwa huko Marekani.
Mwanamke huyo mw enye makazi yake nchini Marekani ameushangaza umma baada ya kujifungua mwanaye wa kike mwenye uzito wa kilo 13 kwa mara ya kwanza ikiwa ni uzao wake wa tano. Mtoto huyo aliyepewa jina la Mia Yasmin amezaliwa leo alfajiri akiwa na urefu wa inchi 22 baada ya mama yake kukaa chumba cha kujifungua kwa muda wa siku tatu. Mama yake Alisha Hernandez alitarajia kujifungua mtoto mwenye uzito wa kilo saba lakini alijifungua mtoto huyo siku ya jumatatu. Binanamu yeka Alisha alisema baada ya kuzaliwa kwa mtoto huyo,aliamua kwenda kwenye hospitali ya watoto kwa ajili ya kumfanyia uchunguzi wa kisayansi na kubaini hana tatizo lolote na kwa sasa yuko katika hali nzuri. Baba wa mtoto huyo Fransisco Garcia amefurahia ujio wa mtoto wake huyo na kusema ameshukuru kupata mtoto wa tano wa kike ndani ya familia yake baada ya kutangulia wengine wanne wa kike ambao ni Britney, Ximena, Yulissa na Yuliana Hernandez.
No comments:
Post a Comment