December 2, 2014

HII NDIO KAULI YA KWANZA YA YULE BINTI ANAEONEKANA KWENYE VIEO AKIMTESA MTOTO


Baada ya story ya yule msichana kwa anayefanya kazi za ndani Uganda kuchukua headlines katika vyombo mbalimbali vya Kimataifa Duniani, leo kipo ambacho amekizungumza kwa mara ya kwanza tangu afanye kosa hilo.

Msichana huyo Jolly Tumuhiirwe ambaye kwa sasa amekamatwa na Polisi amesema sababu iliyomfanya amtese mtoto Arnella Kamanzi, ni kutokana na kuchanganyikiwa baada ya waajiri wake kutompatia pesa ili amtumie baba yake ambaye alikuwa anaumwa.
Amesema anajiona mwenye hatia kwa alichokifanya japo anadhani alifanya hivyo kama njia ya kumkanya mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimuona mama wa mtoto huyo akimpiga kama njia ya kumkanya.
Jolly amelalamika kuwa anajisikia vibaya pale ambapo wafungwa wenzake wamekuwa wakimtenga sana na kutaka kumpiga.

No comments:

Post a Comment