Miaka miwili baada ya kumpoteza mama yao mzazi, mapacha wa kundi la P-Square la Nigeria Peter na Paul pamoja na kaka yao Jude Okoye wamepatwa na msiba mwingine. Wameondokewa na baba yao Mr Okoye aliyefariki dunia Jumatatu Nov.24.
Vyanzo vya karibu vimesema kuwa Mr. Okoye alidondoka akiwa anaelekea hospitali huko jijini Lagos. Inadaiwa kuwa siku chache kabla hajapatwa mauti alifanyiwa upasuaji wa goti na alikuwa akiendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment