November 26, 2014

HUU NDIO UKWELI KUHUSU MWANAUME ANAYEWATEKA WASICHANA KUWAFANYISHA MAPENZI DAR NA KISHA ANAWAUA.



Polisi kanda ya Dar es salaam wametoa tahadhari kwa wanawake kuacha kushiriki mapenzi na watu wasiowafahamu ili kuepuka kuuawa.
Taarifa ya Kamishna wa Kanda Suleiman Kova ilisema wasichana hususani wa jijini Dae es salaam wanatakiwa kuwa makini na wanaume wasiowajua kwa sababu wengi wameishia kuuawa kikatili huku miili yao ikitelekezwa hovyo.

“Kuna taarifa ya kuwepo wanaume wawili wanaowashawishi wanawake kufanya nao mapenzi na baada ya muda huwaua,natoa tahadhari kwa wanawake wote kuwa makini na watu hawa”alisema Kova.


Alisema siku za hivi karibuni kumekuwepo na matukio mengi ya mauaji ya aina hiyo ambapo kwa sasa wanawake wapatao sita tayari wameshapoteza maisha.

No comments:

Post a Comment